Total Pageviews

Wednesday, February 28, 2018

SHULE YETU NAMALEBE: WEWE UMEIFANYIA NINI?

Wana wa Namalebe!
How old are You?
Where are You today?
What are You doing?
Did you know that your Old School, Namalebe is turning 70 Years old next year?
Do you remember where Namalebe have taken you from those Good Old Days to where you are Today?
What have you done to Namalebe in Return!

Wana wa Namalebe,
Let's Go and Tell Namalebe
AHSANTE SANA.

Please make arrangements to attend the Event in June 2019,
You gonna enjoy meeting your Old Colleagues there.
GET PREPARED.


Tuesday, February 27, 2018

KUSHIRIKI SABATO NYUMBANI


Nyumbani ni nyumbani,
Wakati wa likizo yangu nilipata Baraka za kushiriki Sabato Mbili katika kanisa la Nyumbani la Nakatuba.
Tulipata kubarikiwa sana kwa mafunzo mbalimbali, kujifunza Lesson pamoja, Nyimbo na Mahubiri.
Ni Kanisa hili Mzee CK Msalya alikuwa na ndoto ya kuliona likikamilika, lakini muda huenda haraka mno. Ukamilikaji wake ni Changamoto kubwa sana kwa washiriki wa hapa, 
Wazee wa Kanisa walielezea mpango wa kufanya Harambee baadae mwaka huu ili kuendeleza pale palipofikiwa,
Familia ya Msalya pamoja na wadau wa Blog wameombwa kuendelea kutowatupa mkono washiriki wa Nakatuba.
Chochote kidogo kitakachokuwa kikipatikana kikasaidie kunyanyua Juu Kanisa la Bwana Nakatuba. 

Wednesday, February 21, 2018

QUEUING FOR NATIONAL IDENTITY



Nakatuba na Namalebe
Busambara

Zoezi la kuwapatia wananchi wote Vitambulisho vya urai wa Tanzania liko mkoani kwetu.
Nilikuwa Likizo karibuni,
Ni yaleyale ya Dar Es Salaam tulipokuwa na zoezi hilo. Foleni ndefu za kuchosha na mipangilio isiyoeleweka huku kukiwa na Mashine chache za kuandikishia.

EX NAMALEBE STUDENTS

Namhula wakati wa Likizo.
EX Namalebe Student - Bi Rebeka Nyabwire Malekela. (Mrs Yoel Massano)
Ni miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kabisa wa Shule ya Msingi Namalebe wakati inaanzishwa.
Mwaka 1949, na akamaliza hapo mwaka 1952.
Anawakumbuka Walimu wake waanzilishi, Mwl Sylivery na baadae Mtobhesya.
Blogger alipata nafasi ya kumtembelea kijijini kwake Namhula wakati wa Likizo.
Blogger nae ni EX Namalebe Student, aliyeingia 1967. Miaka 15 baada ya Rebeka kuondoka.
Are They School Mates?

Thursday, February 15, 2018

RK BEACH, NYUMBANI MBALI NA NYUMBANI

RK Beach Hotel,
Majita Murangi.
Kiota kipya kabisa kupata kutokea Majita na Musoma kwa ujumla,
Beach safi kabisa,
Mazingira tulivu sana.
Huduma nzuri zenye Hospitality halisia ya Majita.
Vinywaji na Chakula maridhawa.
Hakika RK Beach ni Nyumbani mbali na nyumbani.
Mimi nitarudi tena.

Tuesday, February 13, 2018

HARUSI YA KIKWETU

Harusi ya Kikwetu katika uhalisia wake.
Ina manjonjo na vimbwanga vyake katika hali ya kupendeza,
Misosi na madikodiko lukuki kwa ajili ya wahudhuriaji wote.
Kasuguti, Bunda
Hivi Karibuni

TAHADHARI YA NJAA

Hivi karibuni nilisafiri kwa ajili ya Likizo ya mwaka katika Wilaya za Bunda na Musoma Vijijini.
Chakula kikuu katika wilaya hizi kiasili imekuwa Muhogo na Mahindi, lakini kwa miaka ya karibuni zao la Mhogo lilikumbwa na ugonjwa wa Cassava Meal Bug na kusababisha zao la muhogo kutoweka kwa asilimia kubwa.
Hali hiyo inajitokeza sasa kwenye zao la Mahindi, na kwa kuwa Wakulima wa mikoa ya kanda hii ya ziwa hawana utamaduni wa kutumia viuatilifu kwenye mazao ya chakula, inaelekea hali ya upatikanaji wa Chakula itakuwa ngumu.
Wakulima waliowahi kulima mahindi mwezi wa Tisa na wa Kumi ndio pekee waliofanikiwa kupata mavuno. Waliolima kuanzia Novemba na kuendelea, kwa maeneo yote niliyopitia Mahindi yameshambuliwa na wadudu na hakuna matarijio kabisa ya kuvuna.
Wakulima pekee wenye matarajio ya kupata walau chakula kwa musimu huu ni wale walioweza kulima Mtama na Uwele.
Maofisa Ugani na Serikali bila ya shaka wataliona tatizo hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.