Thursday, December 28, 2017

TEMBEA UJIONEE

Mwanamuziki Nguli nchini, Hayati Remmy Ongala alipata kuimba "Tembea ujionee"
Unaweza kuwa umepata kutembelea Baa za aina mbalimbali, Miti ikiwa imepandwa karibu kuzizunguka au hata ndani yake kwa ajili ya kupendezesha mazingira.
Lakini sivyo kwa "The Big BaoBab Tree Bar" mambo ni tofauti hapa. Baa hii iko ndani ya Mti mkubwa wa Mbuyu, wenye maelfu ya miaka na unaosadikika kuwa Mti Mkubwa kuliko yote Duniani.
Hapa ni katika mji wa Modjadjiskloof, katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini.
Hakika Tembea ujionee........

Source
Mitandaoni

50 th WEDDING ANNIVERSARY


Miaka Hamsini iliyopita,
Naam, Nakubali kukupokea katika Shida na Raha.
Nusu Karne sasa, Uhusiano unazidi kukua na kuwa bora zaidi.
Kila la kheri Bw na Bi Lucas Daniel Gunze.

Recently in Bariadi.

Wednesday, December 27, 2017

TANZIA: MONICA SALANYA HATUNAE

Ndugu yetu, Dada yetu
MONICA SALANYA
Hatunae tena, Amefariki Saa Mbili Usiku wa kuamukia leo Kariuki Hospital alikokuwa amelazwa.
Mipango ya Mazishi inaendelea Nyumbani kwake Kinyerezi.
Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

Sunday, December 17, 2017

17th WEDDING ANNIVERSARY, THE MGABOS

Mwanza, 
Sunday 17th December 2000
Dodoma,
Sunday 17th December 2017
After all these years, you still make an amazing couple. I wish you a very happy wedding anniversary.

Friday, December 15, 2017

Thursday, December 14, 2017

MUNGU NDIYE AJUAE!

Kwa muda mrefu sasa yapata mwezi sasa nikipanga kuipeleka Gari service, hasa kwa hisia za kuwa na kasoro kwenye Usukani.
Jana nilisisitiza kwa Mafundi waichukue, na walifanya hivyo asubuhi.
Huko walikoenda,
Gari imechomoka tairi mitaa ya Goba, Pichani. Hakuna majeruhi.
Hakika Mungu Pekee Ajuae.

KAMBI YA VIJANA KIBIDULA

Kibudula, Iringa
Kambi ya Vijana wa Ki Adiventista Wasabato inayoendelea na imewakutanisha vijana kutoka nchi mbali mbali zipatazo 11.
Mafunzo mbali mbali ya Stadi za kazi na Maisha hutolewa.

Monday, December 11, 2017

ANOTHER GRADUU

Yes, 
Kadri unavyosoma na kusonga, ndivyo unakuwa na nafasi nyingi za kufurahia kuhitimu.
Minoo, ndani ya Miezi Mitatu ana "Graduate" tena.
Lakini hii ni ya kumaliza miezi mitatu ya Pre Form One.
Jumamosi, Muhanga Secondary School

WAIJUA KABILA YA VADOMA

 Kabila ya Wa Vadoma, hujulikana pia kama Dema. Hupatikana Mkoa wa Kanyemba, Kaskazini mwa Zimbabwe kwenye wilaya za Urungwe na Sipolilo.
 Watu wa kabila hili wanakabiliwa na hali ya maumbile ijulikanayo kama "Etrodactyly".
Tatizo hili pia hujulikana kama "Miguu ya Mbuni" na huweza kuathiri Mikono na Miguu.Vidole vya kati hukosekana, na vile vya pembeni hukunjika ndani.
 Tatizo la Miguu ya Mbuni hutokea 1 kati ya 90, Lakini kwa Wa Dema ni kubwa kwa sababu wao wanasisitiza kuoana wao kwa wao tu.
Wa Dema ni waumini wa madhehebu yao ya kiasili au kanisa la Waadiventista Wasabato.

Saturday, December 2, 2017

MTAA KWA MTAA

Kinyerezi yetu,
Mengi yanabadilika,
Ili kuenenda na kujionea mabadiliko,
Maulid Day ilikuwa Kinyerezi Mtaa kwa Mtaa,
na Chochoro kwa chochoro.

Wednesday, November 29, 2017

TAFAKARI KABLA YA KUTENDA

Tafakuri ya Mbuzi kabla ya kuvuka Daraja,
Kigogo Mkwajuni,
Leo Asubuhi

Tuesday, November 28, 2017

KISA CHA KALENDA

Hapo zamani,
Mwaka 1752, Waingereza walipokwenda kulala tarehe 2 Septemba lakini walipoamuka kesho yake ilikuwa tarehe 14 Septemba.
Kulikoni,
Siku 11 zilikuwa zimeondolewa kwenye Mwezi wa Tisa ili kuendana na Sheria mpya ya Kalenda.
"Calendar (New Style) Act of 1750"
Huu ni Mwezi Waingereza walihama kutoka matumizi ya Kalenda ya Julian kwenda Kalenda ya Gregorian.
Pia katika Kalenda ya Julian, mwaka mpya ukianza Tarehe 1 April. Sasa hata baada ya mabadiliko Waingereza wengi wakiendelea kusheherekea Mwaka Mpya April mosi. Kwa kuchukizwa na hilo Mfalme akawa ametoa amri kuwa wote wanaoendelea kusheherekea Mwaka Mpya April Mosi kuitwa Wajinga, Na kuanzia hapo April Mosi imejulikana kama Sikukuu ya Wajinga.

"Kutoka Mitandaoni"