Monday, October 30, 2017

PAULO MJASIRIAMALI

Nakatuba, Jumatatu.
Mjasiriamali Bw Paulo baada ya ndoto za Uinjinia kuyeyuka.

Friday, October 27, 2017

MVUA ZA KWANZA......


Falsafa ya dhati ya Baba wa Taifa, akituhimiza Kilimo kama Uti wa Mgongo.
Naam, mvua za vuli zimeanza Nakatuba,
Ni mwanzo wa msimu wa Kilimo kwa kuwa Mvua za kwanza ni za kupandia.
Nakatuba kwetu.

Thursday, October 26, 2017

NAKATUBA KWETU

Mdau wetu Mzee wa Makamuzi yuko Nakatuba,
Na amekuwa akituhabarisha yanayojiri pande hizo.
We Miss Fresh Sato very much.

Sunday, October 22, 2017

MWANAMME KAZI

Kinyerezi kwetu leo,
“Kila mtu anapaswa kula na kunywa na kufurahia kazi yake yote ngumu. Ni zawadi kutoka kwa Mungu.”

Thursday, October 19, 2017

Monday, October 16, 2017

PAAVO NURMI - SHUJAA WA OLIMPIKI UFIN


Paavo Nurmi,
13 Juni 1897 - 02 Oktoba 1973
Mwanariadha nguli wa Kifini kupata kutokea, akishiriki mbio za masafa marefu na za nyika. Akijikusanyia Medali 12, zikiwemo Tisa za Dhahabu, na Tatu za Fedha.
Mashindano yake ya mwisho yakiwa yale ya Olimpiki ya Amsterdam ya mwaka 1928.
Sanamu yake inashuhudiwa leo pembezoni mwa uwanja wa Olimpiki wa Helsinki.
The Helsinki Olympic Stadium   
Ulijengwa mnamo mwaka 1952, na kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki.
Mnara wake ukiwa na urefu wa Meta 72.71


Thursday, October 12, 2017

KAZI NI KAZI


Our Super Konda kazini,
Kinyerezi Majumba Sita,
Enjoying his job

Tuesday, October 10, 2017

ELECTRICAL CARS CHARGING

Car charging available at Car Parking.
Alvsjo, Stockholm.

Monday, October 9, 2017

ZIARA ATLAS COPCO

Atlas Copco main office in Nacka
Jumanne 03 Oktoba 2017,
Ziara yetu Asubuhi inaanzia Makao Makuu ya Atlas Copco, Nack. Sweden
Hii ni Kampuni kongwe iliyoanzishwa mnamo mwaka wa 1873. Imeenea Duniani kote ikiwa na wafanyakazi wanaofikia 44,000
Hawa ni wabobezi katika uzalishaji wa zana za kutendea kazi viwandani, vifaa vya uchimbaji wa mifumo ya miamba na vifaa vya utengenezaji barabara.
Ni ziara ya kusisimua, inayotupeleka kutembelea machimbo yaliyoko chini ya ofisi kwa mita zipatazo 40.

Sunday, October 8, 2017

PHOTO SHARING FROM UNGUJA



Wadau wetu wa Dodoma na Morogoro walipata nafasi ya kuhudhuria Kongamano la Kina mama wa Ki adventista Wasabato mjini Unguja.
Ilikuwa ni fursa adhimu pia ya kufanya Utalii wa ndani. Kuijua mitaa ya Unguja, Forodhani, Stone Town na mingineyo, Prison Island kwenye Tausi wadogo na Kobe wakongwe, Kuwaona Pomboo wa Nungwi pamoja na sehemu mbalimbali za kihistoria.
Naam, aliimba Remmy Ongala
"Tembea ujionee, usingoje kuambiwa"