Total Pageviews

Tuesday, September 26, 2017

UTII BILA SHURTI


Helsinki,
Nidhamu ya hali ya juu katika matumizi ya Barabara

KAMA BAGAMOYO, KAMA HELSINKI

Zamani za kale niliiona Biashara hii Bagamoyo, Tanzania.
Unakodi Baiskeli unaenda safari zako, ukirudi unalipia kulingana na muda uliotumia.
Nimeiona tena Helsinki, Finland.
Unachukua Baiskeli, unaenda na safari zako. Malipo kwa Kadi yako ya Pesa. Ruhusa kuiacha point nyingine yenye Baiskeli.
Bagamoyo nina hakika Wakodishaji walikuwa hawalipi Kodi,
Helsinki nina Imani wakodishaji wanalipa Kodi.

OUR PET, OUR FAMILY MEMBER

Kwa Wafinn,
Mnyama wa nyumbani wa kufuga, ni Family Member
Kwa hiyo anakuwa na haki zote za wanafamilia,
OUT ni haki yake pia.

MAISHA POPOTE

Cha muhimu Elimu, Maisha ni popote.
Tumekutana huku na Vijana wa Kitanzania,
Wanapiga mzigo kama kawaida na wanaheshimika kwa jamii ya Wa Finn.
Hongereni sana. (Majina Chemba)

AFTERNOON SELF TOUR

Mchana leo imekuwa ni Tour ya kujipangia mwenyewe,
Ni Tour ya kusafisha macho kwa kuutembelea mji wa Helsinki.
Nimepata bahati ya kuwa na mwenyeji, kwa masaa takribani tumezunguka eneo kubwa mji wa Helsinki na kujionea maeneo mbali mbali, Povoo, Mpakani na Estonia, Bandarini, Olympic na Stadium nk
Bw Tor- Gunnar Lindborg, Mwenyeji wa hapa ambae niliwasiliana nae kabla ya kufika hapa alikubali ombi langu la kunitembeza mjini.
Ni mchangamfu na mkarimu sana, amekaa na kufanya kazi sehemu mbali mbali Tanzania kule Moshi, Dar Es Salaam na Mtwara.

STUDY TOUR DAY TWO, HELSINKI FINLAND

Jumanne,
Helsinki, Finland
Ziara yetu imeendelea kwa kukutana na Wafanyabiashara wa Makampuni mbali ya Finland.
Taarifa ya ziara hii imekuweko kwenye vyombo vya habari na mitandao ya hapa Finland.
Tumekutana nao kwenye jumba la FINNPRO hapa mjini Helsinki, ambapo wengi wamejitokeza kuelezea shughuli zao na namna gani wangependa kupata Washirika wa Biashara kutoka Tanzania.
Wachache tayari kwa kutumia Ma Agent, wana shughuli zao Tanzania.

SMOKING AREA

Pahala maalum kwa ajili ya wavuta sigara,
Tukholmankatuz, Helsinki.

USAFIRI WA TRAM MJINI HELSINKI


TRAM,
Ni mfumo wa usafiri wa kipekee hapa mjini Helsinki nchini Finland. Ni magari ya umeme yanayotembea kwenye reli maalum na mfumo huu unaenda sambamba na magari mengine barabarani ukifuata sheria zote za barabara.

TRIPLA - IN THE HEART OF NEW HELSINKI

In the afternoon we visited the On going project in Pasila, The Mall of Tripia.
This is a dream come true of renowned Finnish Architect Gottilieb Elien Saarinen of making Pasila the Heart of New Finland.
The Mall which when completed in 2019/2020 will be the largest shopping centre in Finland and will include a shopping Mall, Offices, Apartments, A Hotel and be the new public transport hub for the Capital City.
The current project works are undertaken by YIT Corporation founded in 1912.
The Project is funded by Insurance Companies and some Investments from EU Banks.