Mwanamuziki Nguli nchini, Hayati Remmy Ongala alipata kuimba "Tembea ujionee"
Unaweza kuwa umepata kutembelea Baa za aina mbalimbali, Miti ikiwa imepandwa karibu kuzizunguka au hata ndani yake kwa ajili ya kupendezesha mazingira.
Lakini sivyo kwa "The Big BaoBab Tree Bar" mambo ni tofauti hapa. Baa hii iko ndani ya Mti mkubwa wa Mbuyu, wenye maelfu ya miaka na unaosadikika kuwa Mti Mkubwa kuliko yote Duniani.
Hapa ni katika mji wa Modjadjiskloof, katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini.
Hakika Tembea ujionee........
Source
Mitandaoni