Total Pageviews

Monday, May 30, 2016

BUNDA UPDATES IN PHOTOS

 Nesi wa zamu
 uchungu wa dawa
Tamu baada ya chungu

PENYE NIA PANA NJIA

Walimwambia hataweza,
Alitumia Tindo na Nyundo,
Miaka 22 baadae aliwadhihirishia anaweza.
 Dashrath Manjhi.1934 -2007
Ni simulizi ya kale ya kweli ya Dashrath Manjhi.
Dashrath Manjhi aliondoka kijijini kwao  Gehlaur katika wilaya Gaya Bihar ya kwenda kufanya kazi za kibarua katika migodi ya Dhanbad, baadae alirejea kijijini na kumwoa Bi Phalguni Devi.
Dashrath akifanya kazi zake mbali milimani na mkewe Bi Phalgun akimpelekea chakula cha mchana. Siku moja katika harakati za kumfikishia mumewe chakula Bi Phalgun alitereza na kuanguka. Aliumia vibaya. Ilikuwa kazi kubwa sana kumfikisha kwenye matibabu katika hospitali ya kijiji jirani cha Wazirganj. Pamoja na kwamba ilikuwa umbali wa kilometa 10 hivi upande wa pili wa mlima ilikuwa ni lazima kuzunguka mlima kwa umbali wa zaidi ya kilometa 40.
Hapo ndipo wazo la Dashrath la kuwa na barabara ya kuwaunganisha na majirani zao lilipoanzia, lakini wanakijiji wenzie walimwona kama mwendawazimu anaewazia jambo lisilowezekana. Waliamini haitawezekana.
zana alizotumia zikioneshwa na mwanae
Dashrath aliweka nia ya kujenga njia ya wazo lake.
Alichukua Nyundo na Tindo, na kwa mikono yake kwa miaka 22 (1960 - 1983) aliweza kutengeneza barabara iliyopunguza  umbali kutoka mzunguko wa Kilometa 55 hadi njia ya mkato ya kilometa 15.
Alijipangia muda wa kutenda kazi hii, akiamuka alfajiri kutenda kazi za shambani kwake, na baadae kutengeneza barabara hadi mawio.

Hatimae alifanikiwa.
Dashrath alifariki tarehe 17 Agosti 2007 kwa maradhi ya kansa ya kibofu katika hospitali ya All India Institute of Medical Sciences (AIIMS), New Dheli na kupewa mazishi ya kitaifa na serikali.
Dashrath Manjhi - "Mountain Man"

SOURCE:
Mitandao

UPENDO WA MAMA

Happy Birthday Rebecca Nyamweya.
A post from Mom 0041 hrs

Sunday, May 29, 2016

BURIANI XAVERY MGOMA

Tumepata nafasi ya kushiriki ibada ya mazishi ya ndugu yetu Xavery  Lwigi  Mgoma kwenye Kanisa katoliki Ukonga na mazishi kwenye makaburi ya Airwing.

Saturday, May 21, 2016

KWA NINI WALITOBOA?

Miaka 20 tokea ilipozama Meli ya MV Bukoba.
Lakini hadi leo bado najiuliza kuhusu wataalamu wetu kwa nini walitoboa eti wapate nafasi ya kuingia na kuokoa watu?
Kwa elimu ndogo ya ueleaji ninayoijua, hewa iliyokuwemo ndiyo ilikuwa ikisaidia meli isizame kabisa, na ingeweza kuvutwa kwa kutumia nguvu ndogo.
Ni mawazo yangu tu............
Wapumzike kwa amani wahanga wote wa MV Bukoba.

Wednesday, May 18, 2016

A COAT FOR A GOAT !

Remember that old goat poem?
“Where are you going my little goat?
I am going to the market to buy a new coat.
A coat for a goat, or a goat for a coat.
People will laugh at a goat with a coat.”

Tuesday, May 17, 2016

Saturday, May 7, 2016

INFANTS ARE ANGELS

Ajali mchana huu Msimbazi centre Kawawa Road.
Gari zote mbili zikitokea Boma kuelekea Magomeni.
Hakuna majeruhi.
Gari ndogo ilikuwa na dereva na mama mwenye kubeba mtoto anaekisiwa kuwa na siku moja au mbili hivi.
Gari ndogo imepigwa ubavuni, ikazungushwa na kuonekana kama zinazopishana.
Hakika watoto ni Malaika.

HAPA KAZI TU

Hapa kazi tu !!
Shikamoo Tanesco,
Ndani ya masaa 12 nguzo zilizoanguka zimerejeshwa.

USAFI DAY

Delmonte leo asubuhi,
Tumetekeleza kwa vitendo maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar Es Salaam ya kufanya usafi.

Friday, May 6, 2016

KIZAAZAA

Ilikuwa taharuki kubwa mitaa yetu asubuhi ya leo,
Nguzo tatu za umeme  zimedondoka Msimbazi Centre, Kawawa Road na kuzua hofu kwa watumiaji wa barabara.
Hakuna aliyejeruhiwa.

Tuesday, May 3, 2016