Ndio maana mara nyingi sipendi kuuangalia mechi zenye ushindani, Pressure ya nini Bana?
Hii ni mechi ya Liverpool na Manchester City Wembley jana usiku.
Hapa kuna Wanazi wa mpira, Man U, Liverpool, Arsenal na Chelsea.
Unaweza kuwatambua yupi ni yupi?
Total Pageviews
Monday, February 29, 2016
Saturday, February 27, 2016
Friday, February 26, 2016
Thursday, February 25, 2016
UTAMU WA SIASA
Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia na kutaka
kumpiga mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake
wakati akitoka mahakamani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Wassira akitoka kwenye jengo la Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu.
Inadaiwa kuwa Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera, lakini hakuweza na baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.
Kwa mujibu wa Jamson (Mpiga picha) alisema Wasira, ambaye amefanya kazi na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na kitendo chake cha kumpiga picha.
“Wasira alinifuata na kuniuliza sababu za kumfuatilia kila mara. Aliniuliza picha nazopiga nazipeleka wapi,” alisema Jamson.
“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako. Hivi mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira.
Wasira hakuishia hapo, katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa barabara.
Awali, Jaji Sirilius Matupa alitupilia mbali maombi ya ruhusa ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kufuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Bunda baada ya kubaini waliowasilisha maombi hayo, Magambo Masato na wenzake wanne, hawakufuata sheria.
Uamuzi huo ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Eugenia Rujwahuka kwa niaba ya Jaji Matupa.
SOURCE:
Mitandaoni

Wednesday, February 24, 2016
NAKATUBA SHOPPING, CONSTRUCTION PROGRESSING
Mwanasheria, Mzee wa Halamashauri, Mzee wa "Bhukoma" yuko Nakatuba.
Na leo ameshuhudia ujenzi unaoendelea wa Proposed shopping centre yetu.
Nakatuba leo asubuhi.
Tuesday, February 23, 2016
Sunday, February 21, 2016
Saturday, February 20, 2016
Friday, February 19, 2016
Tuesday, February 16, 2016
UMEWEKA ALAMA ?
Nimekumbuka leo kisa cha watu wawili waliokwenda pahala kupitia mwitu
mkubwa, Mmoja mwerevu mwingine mpumbavu. Mwerevu wakati wa kwenda alidodosha
vipande vidogo vidogo vya mawe njiani, wakati wa kurudi vipande hivyo
vilimsaidia kutambua njia ya kurudia. Mpumbavu alinyofoa vipande vidogo vidogo
vya mkate na kuvitupa njiani alimopita, Kunguru walividonoa na kuvila, na
wakati wa kurudi hakukuwa na alama yoyote, akapotea mwituni.
Dar Es Salaam nayo inabadilika haraka, kama huna alama zako
huko mjini ipo siku utapotea.
Monday, February 15, 2016
BIASHARA UBUNIFU
Ama hakika biashara inataka ubunifu, Wauzaji mashine za kukatia mbogamboga.
Mtaa wa Swahili, leo mchana.
Mtaa wa Swahili, leo mchana.
Tuesday, February 9, 2016
Monday, February 8, 2016
Sunday, February 7, 2016
MAJI YA SHINGO
Jumapili, masaa yanayoyoma......
Ukiangalia mambo ya Shuler Hayakawa sawa.
Unachohitaji ni elimu ya kujitegemea.
Kinyerezi kwetu, Leo Alasiri.
Ukiangalia mambo ya Shuler Hayakawa sawa.
Unachohitaji ni elimu ya kujitegemea.
Kinyerezi kwetu, Leo Alasiri.
Thursday, February 4, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)