Friday, November 29, 2013

Thursday, November 28, 2013

POZI ZA KIDIGITALI

Enzi zetu zile unaazima saa au shati la ndege kwa ajili ya pozi ya picha,
Sasa hivi pozi ni kijiditali zaidi.
Milly akipozi.........

Tuesday, November 26, 2013

PARANE

Parane Secondary School
Makamanda wangu walipita hapa

Thursday, November 21, 2013

FEEDBACK

Hatimae kilio chetu kimesikika,
Marekebisho yamefanyika jana, na tunapita kwa amani.
Kinyerezi Darajani

Wednesday, November 20, 2013

MTENDAJI ANUSURIKA KIFO AKIDAIWA KUIBA MAHINDI BUNDA.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe
Na Masau Bwire, Bunda.
OFISA Mtendaji wa Kata ya Iramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Simon Katikizu,
amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumshambulia kwa mawe
wakimtuhumu kuiba mahindi ya msaada.
ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi
ya msaada.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Kijiji cha Isanju ambacho 
ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi
ya msaada.
Wakati kazi ya kugawa mahindi hayo ikiendelea, wananchi hao walibaini upotevu wa
magunia zaidi ya 40 na baada ya kufanya uchunguzi, wakagundua wizi huo
ulifanywa na Bw. Katikizu 
hivyo walianza kumshambulia kwa mawe na marungu.
“Tumemkamata na mahindi ya msaada akiwa ameyaficha nyumbani kwake, katika Ofisi
ya Elimu, kilimo na mengine aliyaweka katika nyumba za rafiki zake, wakati
akijaribu kukimbia lilipigwa yowe,” alisema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
CCM, katika kata 
hiyo, Mohamed Gamba.
Alisema Serikali ilipeleka msaada wa magunia 318 ya mahindi
kwa ajili ya vijiji vitano vya kata hiyo ambapo kila kijiji kilipaswa kupata
magunia 63 kutokana na njaa inayowakabili wananchi.
Vijiji vilivyokumbwa na tatizo la njaa ni Isanju, Mugara, Sikiro, Nyarugoma na
Mwiruruma, lakini. Katikizu aliiba kiasi kikubwa cha mahindi ambapo kijiji cha
Nyarugoma, kiliambulia magunia 26 ndipo wananchi walipokuja juu na kugundua
wizi huo. 
Mkuu wa Wilaya hiyo, Joshua Mirumbe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kudai kuwa, tayari amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri amsimamishe kazi, Katikizu
kwa kosa hilo.
“Huyo Ofisa Mtendaji habari zake ninazo, aliwahi kuiba na kuuza mitumbwi 20
iliyokamatwa katika uvuvi haramu hivyo kutokana 
na tukio hili, nimeagiza Mkurugenzi amsimamishe kazi kuanzia 
leo (jana) na ashitakiwe kwa wizi,” alisema Mirumbe.
Alisema viongozi wa namna hiyo hawafahi kuendelea kuongoza na wanaitia doa
Serikali hivyo hawana budi kuondoka wabaki viongozi waaminifu na waadilifu
watakaowaletea wananchi maendeleo. 
“Siko tayari kuona viongozi wezi, wabadhilifu na wababaishaji wakiendelea
kuwanyonya wananchi kwa kuwaibia, kama wapo wajiondoe kabla sijawafikia,
nitaanza na huyo Ofisa Mtendaji 
ili iwe mfano kwa wengine,” alisema.
Majira lilipomtafuta, Katikuzu na kumuuliza juu ya tuhuma hizo alidai madai
hayo ni uzushi uzushi na hakuna wizi wowote aliofanya bali yeye ni miongoni mwa
Watendaji waadilifu wilayani humo wanaoaminiwa kiutendaji na. Mirumbe.
Juma Mtanda
 
Source: Marayetu Blog

Tuesday, November 19, 2013

KUNANI MM HOTEL

Asubuhi hii inavyoelekea hali si shwari pale M M HOTEL, Uhuru Rd karibu na Klabu ya Wazee.
Nimepita hapo nimekuta kundi kubwa la watu wenye nyuso za taharuki,
Kunani eneo hilo?
Tutege sikio.
Uhuru Rd Asubuhi

Monday, November 18, 2013

BABU "BenGeorge" HADHARANI

 Babu Bernard-George "BenGeorge"
 Na Aunt Asnat
 Babu Kagere
 Na Babu
 Na Dad, Bibi, Uncle na Aunt
BenGeorge akiwa na Bibi na Mom.
Babu BenGeorge, jana Kipunguni alipojitokeza kwa ajili ya pozi na wadau mbalimbali

GOMBANIA GOLI

Gombania goli ndio zetu,
Zamani zile, kuwe na kichwa cha Sato.........
Kufanya "timing" ya macho ni lazima utumie akili ya ziada.
Kinyerezi kwetu, Jumapili

MDAU ASNATI

Mdau Asnati
Kipunguni, Jumapili

MPENDE JIRANI YAKO


Jirani ni nani?
Ni yule anaehitaji msaada wako.
Mpende jirani yako

Friday, November 15, 2013

KUTOKA KIJIJINI KWETU

Mtoto anusurika kuliwa na fisi


MTOTO Agnes Mtani (6), mkazi wa Kijiji cha Namarebe, Tarafa ya Nansimo, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara amenusurika kuliwa na fisi baada ya kuvamiwa na mnyama huyo kisha kuokolewa na wasamaria wema. Akizungumza na Tanzania Daima jana akiwa njiani kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, babu wa mtoto huyo, Mnubhi Chiremeji, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12,30 jioni katika kijiji hicho. Kwa mjibu wa Mnubhi, mtoto huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na dada yake aitwaye Mariamu Mtani kwa ajili ya kwenda kuzoa udaga ulioanikwa mwambani, mbali kidogo na nyumba yao. Alisema wakiwa wanatembea kuelekea eneo walikokuwa wameanika udaga huo, ghafla alitokea fisi ambaye alimnyakua mtoto huyo na kukimbia naye. “Baada ya dada yake kuona hivyo alipiga kelele za kuomba msaada na kwa bahati nzuri kulikuwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho alikuwa  jirani, ndipo alipoanza kumfukuza fisi huyo huku pia  akipiga kelele na hatimaye alimdondosha chini, hapo ikawa pona yake,” alisema babu huyo. Alifafanua kuwa baada ya fisi kumdondosha mtoto huyo chini, wananchi wengine walifika na kumkuta akiwa na majeraha usoni, kichwani hadi begani. Aliongeza kuwa walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika Kituo cha Afya Kibara na kupatiwa matibabu ya awali na baadaye kuhamishiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi. Katika siku za hivi karibuni kumezuka wanyama aina ya fisi katika baadhi ya vijiji vya tarafa hiyo ambao wamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi na mifugo.
Chanzo;Tanzania Daima

Thursday, November 14, 2013

NJIANI TOKA SHULE

Huchelewa kurudi siyo kwa ajili ya "Tuition" tu
Wana shughuli nyingi njiani wakati wa kurudi.
Msimbazi Mission, Kawawa Road

Tuesday, November 12, 2013

UJUMBE TOKA KIPUNGUNI

Received
04:33:18
10-Nov-2013
from:
Eddy
+255716207878

Atukuzwe Mungu kwa Upendo na rehema zake.Nyumbani kwetu amezaliwa Mtoto Mwanaume
(BABY BOY) Saa 9:20 Usiku.
Mama na Mtoto wanaendelea vzri.
Amen.

AMA KWELI POMBE SIO CHAI

 Muugwana akaingia kijiweni na kufikia kwenye siti
Kwa raha zake akiuchapa usingizi
baada ya muda, akaona ni wakati muafaka wa kuingia ndani
Hapa ndipo anapaona kama chumba chake
Baada ya kuona mlango haufunguki anatafuta funguo mifukoni
Hazipatikani
Anabakia mwenye mshangao,
Ama kweli pombe siyo chai.

CHUKUA TAHADHARI

fasten your belt before moving

DAKIKA ZINAPOYOYOMA

Saa zinazidi kuyoyoma
Muda wa kanisani umekaribia kabisa
dereva na gari la bibi harusi halionekani...........
Unaweza kuamua kuanza safari kwa mguu.