Source: Kenyanlist
The Korowai, also called the Kolufo.
Deep within the inaccessible jungle of the southeast Indonesian province
of Papua, about 150 kilometres inland from the Arafura Sea, lives the
Korowai tribe – a clan totally isolated from the rest of the world. They
are hunter-gatherers living in a small society of traditional family
ties who need to share all they have in order to survive. Until their
discovery by a Dutch missionary in 1974, the Korowai had hardly any
contact with the outside world.
The Korowai people live in tree houses ranging in height from 6 to 12
meters, but some are as high as 35 meters above the ground. Usually the
houses are built on a single tree but frequently the base of the house
consists of several living trees, and additional support is derived from
wooden poles. These tree houses protect families not only against
swarms of mosquitoes below, but also ward off annoying neighbours and
evil spirits.
Wednesday, May 29, 2013
HABARI MBAYA TOKA KASAHUNGA NIIJUAYO
Source: Lewis Mbonde Blog (27.05.2013)
VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA NA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA
MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasahunga kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Pia
watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba
walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza
nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.
Kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga
alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa tangu
azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za
usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo
wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo.
Wakiwa kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa kijiji hicho ambao
hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao
kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo
za kinyama.
Wa
kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye
alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo
walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla
ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua
nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile.
Baadaye
walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama
kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa
kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye
kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia
ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu.
Bibi
wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo,
lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga
kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo
kuwachoma na kuwala kwa hasira.
Kamanda
wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo
la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka
waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.
Posted by Lewis Mbonde
Tuesday, May 28, 2013
NANI ATAMKAMATA
Nani amfunge Paka kengele?????
Ni kosa kisheria kupanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu,
Lakini je? anapopanda msimamizi wa sheria za barabarani.....
Nani wa kusimamia tena sheria!
Ni kosa kisheria kupanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu,
Lakini je? anapopanda msimamizi wa sheria za barabarani.....
Nani wa kusimamia tena sheria!
Thursday, May 23, 2013
Wednesday, May 22, 2013
Friday, May 17, 2013
Thursday, May 16, 2013
NJIA ZETU USWAZI
Uswazi kwetu
mpaka ukatize vichochoro uikute barabara ya lami ya kwenda mjini ni kazi kwelikweli,
Madimbwi, mifereji ya maji taka, taka zilizozagaa, matope..........
yaani wee acha tu, Kwetu mradi siku moja inapita inaingia ingine.
mpaka ukatize vichochoro uikute barabara ya lami ya kwenda mjini ni kazi kwelikweli,
Madimbwi, mifereji ya maji taka, taka zilizozagaa, matope..........
yaani wee acha tu, Kwetu mradi siku moja inapita inaingia ingine.