Monday, October 29, 2012

TANZIA - KULWA MALEMBO CHIKONI

KULWA MALEMBO CHIKONI
Baada ya kupigana na kwa takribani mwezi na tatizo la Sukari, Bp, Stroke na siku mbili tatu zilizopita Kwikwi.Hatimae Mdau Kulwa Malembo Chikoni hatunae.
Malembo amefariki jana usiku majira ya saa tatu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe.


Saturday, October 27, 2012

IDD NA VITI VITUPU

Wadau wengi jana Idd imetukuta pabaya
Kijiweni kwetu viti vilikuwa vitupu
Sijui watu baada ya kuwa wamechinja walishushia nini.......
Ilimradi sikukuu yenyewe imepita salama.
 

MITIKO YA IDD USWAZI KWETU

 
 
Watoto walijimwagamwaga mitaani kusherehekea Idd El Haji.
Ni sikukuu ya kuchinja, hivyo bila ya shaka walikwisha pendeza.
Uswazi kwetu Kinyerezi jana

Thursday, October 25, 2012

CYCLING IN DAR

 
Cycling in Dar
Not only for avoiding monotonously queques,
But also for your health.
However ride with extreme care.

USWAZI NDIO ZETU

Hata kwetu Uswazi tuko LIVE
Juzi, kwetu Kinyerezi

UJASIRIAMALI

Ujasiriamali,
inatakiwa uthubutu
Kwetu Kinyerezi, Jumatatu

Wednesday, October 24, 2012

MITAA YA KWETU HII

Mitaa ya kwetu hii
Kinyerezi, Barabara ya Kifuru
Kando ya shule ya Sekondari Ari
Pouda siyo mchezo
Juzi jumapili Kinyerezi

MNAZI MMOJA STAND HAPA

 Stendi ya Mnazi mmoja
Temeke, Buguruni, Kigogo, Gongo la Mboto unapata basi hapa

LUNCH TYME


Lunch Tyme mjini kati
Chakula maarufu zaidi, Chips Mayai
 Nkurumah Street, Jumanne




BONGO NA VIKWANGUA ANGA


  Ushirika Building
 Previously Nasaco offices 
 RITA, Makunganya

Ushirika, Lumumba
Vikwangua Anga kila uchao vinazidi kumea Bongo Darisalama
Ni vyema kuzuru jiji mara kwa mara.

MDAU KAONA

Bi Happy
Mdau wetu Silla kaona.
Na juzi jumapili akisindikizwa na wadau, akiwemo Chief Photographer walikwenda kujitambulisha.
Blogger ameachiwa kazi ya kupeleka "Kibanda".
Ni jambo la kheri, na Blog inawatakia kila la Kheri katika makusudio yenu wadau Silla & Happy


Friday, October 19, 2012

MACHWEO

Kunapokuchwa,
Hata Kunguru hurejea masikani kupumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.
Buguruni Shule, jana jioni

HII IMEKAAJE?

Hii imekaaje wadau?
Kwa wale waliopitia JKT, na mageshi mengineyo.....
Mwenye Rank kubwa anapaswa kukaa kulia.
Lakini sivyo kwa Askari hawa,
Sajenti na Mgambo nani zaidi?

Thursday, October 18, 2012

KWETU USWAZI

 
Kwetu Uswazi, huu ndio usafiri wetu wa kila siku.
Kinyerezi - Majumba Sita
Kinyerezi jana usiku

HEPIBETHIDEI YA MDAU NEEMA

 Msosi
 Vinywaji
 Keki
 Mdau Neema
Wadau wengi walihudhuria
Kama nilivyoahidi Blogger wenu nilihudhuria kuwawakilisha.

Wednesday, October 17, 2012

BLOG YAKO INA MUONEKANO MPYA

 
 
Blog yako sasa iko katika muonekano mpya.
Kutokana na mambo ya kitekinolojia yanavyozidi kubadilika,
Blog yako nayo imeamua kujivua gamba ililozaliwa nalo.
Hopefully utaipenda.
Na sasa kwa kila posts unaweza kuonyesha reaction yako.
Karibuni tuliendeleze libeneke la Blog yetu