Lengo kuu ilikuwa kufanya Chiaz, |
Mapacha |
Sila Msalya
Sarah Msalya
Bright Msalya
Beria Msalya
Billy Msalya
Eddyson Hamis Msalya
Joshua Malembo (Kitukuu)
Kila mtu alifurahia siku hii, sina hakika kama kuna ambae hakuongeza siku kwa kucheka.
Mjadala uliotawala ulimhusu Msalya
kwa wenye kumbukumbu nzuri, wanasema Msalya hakuwa mvutaji wa Sigara, isipokuwa Bangi ya Kibuyu.
Msalya alikunywa pombe kwa nadra, mara nyingi alipokaa na wageni wake maalaum kwa maongezi kama leo vile ndiyo ungemwona akipata ile pombe ya kutumia mrija.
Vipi wanae walikuja kuwa watumiaji wazuri wa Kibuku na Fegi??
Hata hivo wanae hawa nao sasa si watumiaji.
Wakati Msalya anaondoka 1966, kwenye kikao hiki cha leo ni watu watatu tu walikuwa wameshazaliwa.
Msalya alikuwa kiongozi wa Kikundi cha ngoma za asili. kumbukumbu ya ngoma zake imekuwepo nyumbani kwa muda mrefu.
Wadau wanasema pamoja na kuwa si wanae au wajukuu waliorithi mambo hayo,
kuna kitukuu wake ameamua kufuata nyayo zake.
PENINA BILLY
ameamua kuboresha kwa kujiunga na chuo cha sanaa Bagamoyo.