Jioni moja wakati wa kutoka ofisini tunamkuta mheshimiwa huyu nje kwetu. Haijulikani imekuwaje yuko chini namna hii? Kaanguka au namna gani hatujui............. Wasamaria wema wakawepo kumsikiliza na kumsaidia. Akasema anakaa mitaa ya Kawe, anatokea mitaa ya Machinga kumtafuta jamaa yake ampe hela ya dawa maana anaumwa. Kufika hapa kaishiwa nguvu kaanguka. Wasamaria wema wanamuuliza kama amekula au la.... Anasema hajala, lakini shida yake kubwa yeye kwa kuwa anaumwa anaomba Shillingi elfu tatu tu ili akapime Malaria hospitali. inakuwa mtihani kwa wasamaria........................... Hata hivyo wasamaria wengine wanajitolea kumnunulia soda. itamfaa labda kidogo kupata nguvu akisubiria kupata msaada wa shillingi 3,000/= za kupimia malaria
Kesho yake tunahadithiwa alipata mfadhili wa shillingi 5,000/=, na baada ya kuzipokea alipata nguvu za kurudisha chupa tupu ya soda pale ilipokuwa imenunuliwa na wasamaria wa mwanzo.
Jana ilikuwa ni siku ya kikao cha ndugu, "CHENDANE FOUNDATION" kule kwetu Kinyerezi kwa Bw Jackson Kaigi. Na wajumbe wakajimwaya mwaya na Pilau na Soda.
Lakini kumbe jana ilikuwa siku maalum.
Birthday ya
MIKOLINA JACKSON KAIGI
08 JANUARY 2012
Mdau Miko alinaswa mapema asubuhi akihangaikia mahitaji ya shughuli yenyewe Shopping asubuhi ilikuwa ya nguvu
Mdau MIKOLINA
HAPPY BIRTHDAYMIKOLINA JACKSON KAIGI
Mdau pia ana maandalizi wiki hii ya kujiunga na Darasa la TISA, "KIDATO CHA KWANZA" pele Sekondari yetu ya Kinyerezi.
Pamoja na mdau Mikolina.
Jana pia ilikuwa siku ya Chief Blogger ambako ametimiza miaka kadhaa
Simulizi na kumbukumbu zinatuelekeza kwamba alizaliwa tarehe 04 Januari 1932 Kwa maana hiyo Jana 04 Januari 2012 ilikuwa ni siku kubwa kwa Mdau Mkubwa CRAWFORD KULWIJIRA MSALYA MASEME