Monday, October 31, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - NIGHT AT PIDA

Siku ya tatu Bunda,

Spare haijapatikana ikalazimu convoy kujisalimisha PIDA.

PIDA - neno kutokana na "Public Works Department"

zamani zile wakishughulika chini ya Idara ya ujenzi kuangalia matengenezo ya barabara kwa ukaribu. Naikumbuka PIDA ya pale Kasahunga.

Vijumba vyao vilivyochoka ile mbaya vingaliko, ila Pida ya hapa Nyamikoma sikuiona.

Labda kwa sababu niliingia usiku na kutoka alfajiri. Pamoja na kuwa usiku, waheshimiwa hawakusita kupata japo kumbukumbu za blog

Mr Maingu Baruku K Msalya Mr Msalya Baruku Msalya K Msalya

Mwl Belly Snr (ikumbukwe sasa kuna Belly Jnr)
Picha ya kuzama kwa mwezi, Alfajiri tayari kwa safari ya kutafuta spare Rocky City
Bango la shule
Nikaambiwa hili lilitolewa kama zawadi baada ya Mhe. Jovin "Baloteli" wakati akiwa mwanafunzi wa darasa la sita hapa Nyamikoma, kushinda shindano la uandikaji na usomaji wa Insha kuhusiana na vita dhidi ya Malaria.

Customs check point
waheshimiwa wakisaka msosi asubuhi na mapema

Baada ya kushinda Mwanza kutwa nzima nikizunguka kutafuta spare bila mafanikio, nikapata nafasi ya kuwapa Hi kule Shamariwa - Igoma.
Robert, Eddy, Phares na Heri

Mr Phares

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - BUNDA BREAKDOWN

Hakuna namna ya kuondoka.Lazima spare ipatikane, irudishiwe ndipo safari itaendelea. Zilikuwa siku nne za kujionea mambo mbalimbali

God's Garage team.
Mujungu (right), Jita (not in photo) and a number of trainnee assistants
Hii nikaipenda, Ubunifu wa mjasiriamali mmoja Bunda.
Pictures and useful Quotes are sold along Nyerere Rd

Bunda,Opposite Gereji ya God ndio ikawa meeting point yetu na jamaa na ndugu mbalimbali.
Super Mteki alifika kutuona



Father Mwayai, muda mwingi alifika kutujulia maendeleo ya shughuli yenyewe ya matengenezo. wakati mwingine tukapata na nafasi ya ku peruzi

Kumbe hata kwetu Bunda, Gari za watalii hupita,mojawapo ikiishia ishia from Musoma to Mwanza


Tukawa part and parcel ya kijiwe hiki, stand ya Vi "Noah" kwenda Musoma

Nyamasisis walitutembelea pia

Kijiweni kwetu kuna wakati palikuwa hot............

Only in Bunda.........Paka Maalum mwenye shughuli maalum ya kulinda panya dukani, akipokea maelekezo maalum kupitia mlango maalum

Sunday, October 30, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - MWANZA TO BUNDA

Safari inaendelea, kabla ya kuanza. Picha ya kumbukumbu
AIC Makongoro Hostel
Tribute to Mrs Restitutor Lukiko
Kiseke Gravel Yard.

Upumzike kwa amani Restituta "Mama Florah"
Nyakato, Shule ya msingi Gideli tunapita kumpa Hi Father Goodluck Chausi.Furaha ilioje......
Kujiweka sawa kwa safari, Convoy inapata kiamsha kinywa Igoma
Supu ya mbuzi, Chai ya Maziwa, na Chapati.
Igoma hakuna matata......................................
8 Kilometers, before Magu kadhia inaanzia hapo,

Tatizo kwenye Engine??
ndivyo inavyoelekea
Tunajikongoja hadi Magu, Msilanga Garage
Option ya kwanza Changing Oil.
Baada ya masaa kadhaa safari inaendelea kwa kujikongoja, maana bado Gari haiko sawa.
Lamadi.
Kila panapo fursa inapewa maji.
Lamadi
CN Hotel Bunda
CN
Gereji ya God,

Hatimaye tatizo limegundulika, Overheating imeunguza Cylinder Head Gasket

Saturday, October 29, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - ROCKY CITY

Stop Over at Rocky City
Jovin anajiunga na msafara pale Nyegezi Bus Terminal
na baadae Lawyer pale round about ya CCM mkoani
Na route inaelekea Bugando Hospital kumwona Mheshimiwa Lucas Daniel Gunze.Take Note, Shorts and Trousers for females are not allowed at Gate entrance. Lucas & Lawyer Mrs Lucas (Centre)

Lawyer, Grace and Titus


Baadae safari ikaelekea Pasiansi kwa Major Selestine Lukiko.

Huko tunapata picha moja ya kumbukumbu sana.Ni picha yao wakiwa mafunzoni Germany, na mmojawao ni Mkuu wa sasa wa "Geshi" la njii hii. Standing from left (5) David Mwamnyange


From there ni wakati wa kupumzika.

Hapa tunapata somo namna ya ku "make"Room moja pale AIC Makongoro Hostel inatosha kutu "accomodate" Mwanasheria, Makubhi, Jovin "Baloteli" na Mr Blogger kwa ajili ya kupitisha siku kwa gharama ya Tshs 10,000

Mr Blogger & Baloteli

Mzee wa Makamuzi

Friday, October 28, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - DOM TO MZA

Siku njema hunekana asubuhi.
Pamoja na safari iliyopo mbeleni mwetu leo tuliamukia Break fast ya nguvu
Wenyeji wetu awlikuweko kutuona tukianza safari na kutupa mkono wa kwaheri Driver in charge, Mr Makamuzitulivuka milima na mabonde tukiwapita mmoja baada ya mwingine
tukizipita madhari za kila aina
Kila mara tukiangalia alama zilizopo barabarani, tukalinganisha na ramani yetu ya safari.
Tukijionea namna mbali mbali za ubebaji wa mizigo.
Kama huyu jogoo aliyeweka juu ya mkaa, na kufungwa nyuma ya lori, yumkini kumuepusha na athari za upepo mkali.
Tinde
Kizumbi, outskirts of Shinyanga town

ikabidi kusimama kupata picha ya kumbukumbu angalau ya bango la chuo changu nilichokuwepo miaka ya 1980/81
Kizumbi
Shinyanga Hotel,
enzi zake usiombe, ndiyo ilikuwa Hotel ya watu wazito miaka hiyo.
lakini leo imechoka ile mbaya.
Tulisimama hapa baada ya kupata pancha, tukaonelea tupate matengenezo hapa na msosi kabla ya kuendelea.

Nyegezi round about ikatukaribisha kufika kwetu Mwanza.

Rocky City