Picha ya Nyamweya mwishoni mwa miaka ya 90 kama sikosei.
Alifariki mwaka 2002 akiwa ameshavuta zaidi ya miaka 95.
Katika kumukumbuka mtu huyu muhimu sana kwetu, na katika kujaribu kutunza kumbukumbu yake kwa kina Rebeca wajao, Mwalimu Maclaud anaandaa siku maalum ya REBECA NYAMWEYA siku ya tarehe 12.12.2010 huko KARUKEKERE.
Wajukuu wote wanatakiwa kuweko huko wakiwa na familia zao zote.
Watu wote wanashauriwa kuandaa usafiri wao binafsi, angalau kuwepo Karukekere siku moja kabla.
Kutakuwepo na kongamano na maelezo kutoka kwa watu waliokaa na Rebecca na kufahamu historia yake.
Mmepata kusikia kusikia jinsi alivyokutana na waume zake, Magoti I na Magoti II.
Nafasi yako kati ya nafasi adimu zipatikanazo kuhifadhi kumbukumbu hii.
Picha hii ilipigwa na Magoti III